Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwenye nywele bandia zinazotambulika kwa Heading 6704.
Dk Mwigulu amesema hayo bungeni leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha makadilio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Serikali 2022/23
Amesema “Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwenye nywele bandia zinazotambulika kwa Heading 6704.
Hatua hii inalenga kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na kuongeza mapato ya Serikali” amesema
Amesema hatua hiyo inalenga kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na kuongeza mapato ya Serikali