Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushuru magari chakavu wafikia asilimia 10

Fedhapic Ushuru magari chakavu wafikia asilimia 10

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaanza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 10 katika magari ya abiria yanayoingizwa nchini yanayozidi umri wa miaka mitano (magari chakavu).

“Hatua hiyo inakuja ili kuwianisha na magari mengine yanayofanana yanayotozwa ushuru huo. Magari hayo ni yale yanayotambuliwa kwa H.S Codes 8702.20.22, 8702.20.29, 8702.20.99, 8702.30.22, 8702.30.29, 8702.30.99, 8702.40.22, 8702.40.29 na 8702.40.99,”amesema

Dk Nchemba ameyasema hayo leo Alhamis Juni 15, 2023 akiwasilisha hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live