Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushauri wa TICTS kwa wateja juu ya kutoa mizigo bandarini

Ca7c22f42242e3dd923c3ffd96c2e9b5 Ushauri wa TICTS kwa wateja juu ya kutoa mizigo bandarini

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KAMPUNI Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Shehena za Kontena Bandarini (TICTS), imewataka watumiaji Bandari ya Dar es Salaam kuchukua mizigo yao kwa wakati ili kutoa nafasi kwa watumiaji wengine wa bandari kupokea mizigo yao.

Bandari ya Dar es Salaam inakabiriwa na changamoto ya ufinyu wa nafasi, inayopelekea migizo kuchelewa kutoka bandarini hapo kutokana na wateja wengi wa nchi jirani kushindwa kuchukua mizigo yao kwa wakati.

Akizungumza katika ziara ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mkurugenzi wa Mahusiano wa TICTS, Donald Talawa alisema hiyo ni changamoto ila kikanuni ni lazima mizigo hiyo ibaki bandarini.

Alisema asilimia 55 ya mizigo inaingia nchini na asilimia 45 inatakiwa kusafirishwa kwenda nchi jirani kwa kuzingatia kuwa eneo la kontena lina hekta sita tu, ambalo lina uwezo wa kuhifadhi kontena 18500.

Alisema urefu wa eneo namba 8 hadi 11 ni mita 725 ambalo lina uwezo wa kuweka meli tatu zenye wastani wa mita 220, lakini kama meli ina mita kuanzia 220 zinatia nanga meli mbili pekee.

“Kwa wastani tunaweza kusema katika hizi berth nne tunaweza kuweka meli tatu ila kwa wastani kwa leo tumeweka meli mbili kwa sababu kuna matengenezo yanaendelea, hii ilitokana na baadhi ya Piles kuhatarisha maisha ya watu”alisema Talawa.

Alisema kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, ‘Gross’ imekuwa kwa asilimia nne, hii ni kutokana na mizigo kuongezeka, lakini changamoto kubwa ni berth ambazo zimekuwa hazitoshelezi na kwamba kwa sasa wanahitaji berth zingine tano mpaka sita.

Chanzo: www.habarileo.co.tz