Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usajili wa VICOBA waanza ngazi ya halmashauri

VICOBA Usajili wa VICOBA waanza ngazi ya halmashauri

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT, vikundi vinatakiwa kuwasilisha maombi ya usajili katika halmashauri husika ili yafanyiwe kazi na mamlaka husika.

“Aprili 30, mwaka huu, ndiyo mwisho wa kupokea maombi ya usajili kwa vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za kifedha vilivyokuwa vikifanya shughuli zake. Kikundi kitapata changamoto kufanya usajili kwa njia ya kielektroniki, inashauriwa kipeleke maombi hayo kwa Afisa Maendeleo ya Jamii aliyeko katika ofisi ya kata au halmashauri iliyo karibu kwa ajili ya msaada zaidi,” imefafanua taarifa hiyo.

“BoT kwa kushirikiana na TAMISEMI inavitaarifu vikundi (Vicoba) kuhakikisha kuwa vinawasilisha maombi ya usajili kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa husika kabla ya tarehe 30 Aprili 2021,” imesema taarifa hiyo.

Chanzo: ippmedia.com