Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usaili ajira Utumishi wa Umma kufanyika kila mkoa

Mhagama Bungeni K Usaili ajira Utumishi wa Umma kufanyika kila mkoa

Sat, 25 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ameaiagizasekretarieti ya ajira kuhakikisha mfumo wa usaili wa ajira unakwenda mikoa yote nchini.

Akizungumza Bungeni jijini Dodoma Jenista amesema makundi mengi ya vijana hufunga safari mpaka Dodoma kwaajili ya kufanya usaili wa ajira ambapo wanaweza kufanya usaili huo wakiwa mikoani mwao.

"Makundi ya vijana yanasafiri kutoka mikoa mbalimbali kila mara, wanakusanyika hapa Dodoma kwa ajili ya kufanya usaili, tumesikia kilio hicho. Tumefanya maamuzi, mara baada ya bajeti hii kupita, nawaagiza sekretarieti ya ajira kutekeleza maagizo ya Serikali na Mhe. Rais kuhakikisha mfumo wa usaili sasa unakwenda katika mikoa yote nchini" amesema.

Aidha, Mhagama amesema kuna haja ya kuwepo kwa 'database' (kanzidata) ili kuondoa usumbufu kutokana na kuwepo kwa wingi wa ufaulu wa vijana wa kitanzania lakini nafasi zinakuwa chache katika sekretarieti ya ajira.

Amesema kupitia kanzidata hiyo, waliofanya vizuri lakini wakakosa nafasi, watazingatiwa kwanza panapotokea nafasi mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live