Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usafirishaji bidhaa Falme za Kiarabu wapungua

A3de12facce35ec3f4c7c8f09b3c0760.jpeg Usafirishaji bidhaa Falme za Kiarabu wapungua

Tue, 18 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BENKI Kuu ya Uganda imesema usafirishaji wa bidhaa katika nchi za Falme za Kiarabu umepungua kwa wastani wa asilimia 12 kutokana na kushuka kwa mauzo ya dhahabu.

Ripoti ya benki hiyo iliyotolewa Mei 4, mwaka huu inaonyesha kuwa, mapato ya kuuza nje kuanzia Machi yalipungua hadi kufikia dola za Marekani milioni 444 (Sh trilioni 1.642 za Uganda) kutoka dola milioni 447 (Sh trilioni 1.653 za Uganda) Februari, mwaka huu.

Dhahabu ambayo ni bidhaa inayoongoza kwa kuuzwa nje katika nchi za Falme za Kiarabu ilipungua wakati huo hadi kufikia dola za Marekani milioni 155 sawa na Sh bilioni 73 za Uganda kutoka dola milioni 175 (Sh bilioni 647) mwezi Februari.

"Hiki ni kiwango kidogo nchi ilifikia katika usafirishaji wa dhahabu kutoka dola za Marekani milioni 126 Mei, mwaka jana," ripoti hiyo ilisema na kubainisha kuwa usafirishaji katika nchi za Mashariki ya Kati ulikuwa dola za Marekani milioni 160, ikipungua kutoka dola milioni 179 mwezi Februari.

Mchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Makerere Shule ya Uchumi, Dk Fred Muhumuza alisema kushuka huko kunatokana na ushindani wa bidhaa na nchi za ukanda huo zenye mikakati ya kudhibiti usafirishaji wa dhahabu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Alisema usafirishaji wa dhahabu wa Uganda kwa miaka mitano iliyopita umekuwa ukiongezeka na kufikia Sh trilioni 7.6 katika kipindi kati ya Februari, mwaka jana na Februari, mwaka huu.

Dhahabu kwa sasa ni takribani asilimia 50 ya mapato yote ya mauzo ya nje na kwa kiasi kikubwa ikiuzwa katika nchi za Mashariki ya Kati hasa Falme za Kiarabu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz