Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Urusi yasitisha usambazaji wa gesi Finland

Russia Fuel.jpeg Urusi yasitisha usambazaji wa gesi Finland

Sat, 21 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Urusi imesitisha usambazaji wake wa gesi asilia kwa Finland, kampuni ya nishati inayomilikiwa na serikali ya Finland ya Gasum imesema.

Finland imekuwa ikikataa kulipa vifaa vyake kwa sarafu ya Urusi rubles. Lakini pia ni kufuatia taarifa za Finland kuwa itaomba uanachama wa Nato.

Kampuni ya Gasum ilisema hatua hiyo ni "ya kusikitisha" lakini ikasema hakutakuwa na usumbufu kwa wateja.

Licha ya mzozo wa Ukraine, Urusi inaendelea kusambaza gesi kwa nchi nyingi za Ulaya.

Baada ya mataifa ya Magharibi kuiwekea vikwazo Urusi kutokana na vita hivyo, Urusi ilisema nchi "zisizo rafiki" lazima zilipe gesi kwa kutumia sarafu ya Urusi, hatua ambayo Umoja wa ulaya ilichukualia kama kulazimisha kwa kutoa vitisho.

Kutegemea nishati ya Urusi ni sababu inayochangia katika kupanda kwa gharama za maisha kunakowakabili watumiaji wengi.

Finland inaagiza gesi yake nyingi kutoka Urusi lakini gesi inachukua chini ya kumi ya matumizi ya nishati nchini humo.

"Inasikitisha sana kwamba usambazaji wa gesi asilia chini ya mkataba wetu wa usambazaji sasa utasitishwa," Mkurugenzi Mtendaji wa Gasum Mika Wiljanen alisema.

“Hata hivyo, tumekuwa tukijiandaa kwa umakini kukabiliana na hali hii na kwa kuzingatia kwamba hakutakuwa na usumbufu katika mtandao wa kusambaza gesi, tutaweza kuwapa wateja wetu wote gesi katika miezi ijayo,” aliongeza.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, msemaji wa Kremlin alisema "ni dhahiri kwamba hakuna mtu atakayepewa chochote bure".

Siku ya Jumapili, Urusi pia ilikata usambazaji wa umeme kwa Finland. Ikiitishia kulipa kisasi iwapo Finland itajiunga na Nato.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live