Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Urusi kupiga marufuku 'cryptocurrency'

Aaaa9321784bfe89f53b25cf347e410a.jpeg Urusi kupiga marufuku 'cryptocurrency'

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki Kuu ya Urusi inampango wa kupiga marufuku sarafu-fiche (cryptocurrency) kutokana na kuongezeka kwa idadi ya miamala ambayo inadaiwa kuwa hatari kwa utulivu wa kifedha kwa nchi.

Rasilimali za kidijitali zina hadhi ya kisheria nchini Urusi lakini haziwezi kutumika kama njia ya malipo, kwa kuwa serikali inaamini zinaweza kutumika katika utakatishaji pesa au kufadhili ugaidi.

Kulingana na Reuters, benki kuu sasa inajadili uwezekano wa kupiga marufuku na wadau pamoja na wataalam. Ikiidhinishwa, masharti hayo yatatumika kwa wateja wapya wa sarafu-fiche na sio kwa waliopo.

Msimamo wa sasa wa Benki Kuu ya Urusi ni "kukataliwa kabisa" kwa sarafu za kidijitali.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa lilipoiendea benki hiyo kwa ajili ya kutoa maoni yake, ilisema inatayarisha ripoti ya ushauri ili kutoa msimamo wake kuhusu suala hilo.

Kulingana na benki kuu, kiasi cha kila mwaka cha miamala ya sarafu-fiche inayofanywa na raia wa Urusi ni dola bilioni 5. Katika mapitio ya utulivu wa kifedha iliyotolewa mwezi uliopita, mdhibiti alisema Warusi walikuwa kati ya washiriki wengi duniani katika soko la sarafu-fiche.

Mnamo Oktoba, naibu waziri wa fedha wa Urusi, Alexey Moiseev, alisema hakuna mipango ya kupiga marufuku ununuzi wa fedha za kidijiti nje ya nchi au matumizi ya pochi za crypto za ng'ambo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live