Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Urafiki wa mashaka wakwamisha ubia

20888 Simbaye+pic TanzaniaWeb

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye amesema changamoto kubwa katika ubia kati ya Serikali na sekta binafsi ni kutoaminiana.

Ametoa kauli hiyo leo usiku Alhamisi Oktoba 4, 2018 akichangia mjadala katika Jukwaa la Fikra la Mwananchi linalolenga kujadili fursa, changamoto na ufumbuzi kuelekea uchumi wa viwanda ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na kurushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV.

Simbeye amesema Tanzania imekuwa na ubia huku sheria zikibadilishwa kila mara, lakini hakuna miradi ya aina hiyo inayotekelezwa.

"Tatizo kubwa linalokwamisha miradi ya ubia ni upatikanaji mitaji ya muda mrefu. Waziri umekuwa ukifanya kazi ya kutatua changamoto mbalimbali, tunaomba utumie muda wako kubuni vitu vingine vipya," amesema Simbeye.

Amesema wataalamu mbalimbali wanasema Tanzania ina fursa nyingi na kuhoji kama kweli zipo  sekta binafsi inaziona na kuzifanyia kazi?

Amesisitiza kwamba sekta binafsi nchini inakabiliwa na changamoto nyingi, hivyo kuitaka Serikali  kuendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kuhakikisha mitaji ya muda mrefu inapatikana kwa sekta binafsi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz