Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upupu wageuka dili, 1Kg ni Tsh.12,000

Upupu Biz Dili (600 X 341) Upupu wageuka dili, 1Kg ni Tsh.12,000

Fri, 1 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara Josephat Ngamila, amejitokeza mtaani na kutangaza kununua mbegu za upupu na kuusafirisha mpaka Zanzibar kwa shughuli za kuzalisha malighafi, ambazo inadaiwa ni tiba kwa binadamu.

Ngamila amesema kuwa kwa sasa ameamua kuweka soko hilo katika Halmashauri ya Mpimbwe Kata ya Usevya, ambapo ananunua mbegu hizo kwa kiasi cha Sh 12,000 kwa kilo moja.

"Tajiri wangu ambaye ni mwekezaji aliyenituma kazi hii yupo anahitaji tani za kutosha, mbegu hizi inasadikika kuwa zinafanya kazi ya kuongeza nguvu ama uwezo wa mama mjamzito kupata uchungu zaidi,"alisema Ngamila.

Baadhi ya vijana wamechangamkia fursa ya kutafuta mbegu za upupu na kwenda kuzisaka porini, huku wakisema kuwa wakati wa kuzisaka mbegu hizo hukabiliana na changamoto ya kuwashwa mwilini.

"Baada ya kupata taarifa sisi tukaona hii ni fursa, tukaingia msituni kutafuta tukapata kiasi cha kilo 39 kwa muda wa siku nne "alisema Godfrey Kayaya mkazi wa Kata ya Usevya.

"Upupu unawasha kwelikweli na ni kazi sana, lakini nilivyosikia bei ni nzuri nilishawishika kuingia msituni kuzisaka mbegu za upupu,"alisema Mwenda Sadoki mkazi wa Kata ya Usevya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live