Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upakuaji kontena Bandari Dar kuongezeka

62238 Tpapic

Wed, 12 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Isack Kamwele amezindua ghati namba moja katika Bandari ya Dar es Salaam itakayoongeza uwezo kupokea kontena za mizigo.

Akizungumza  leo jioni Jumanne Juni 11, 2019  Kamwelwe amesema kabla ya ghati hiyo kuwepo, walikuwa wakipokea kontena 2, 000 hadi 2,800.

Amesema baada ya kuanza kazi kwa ghati hiyo yenye urefu wa mita 191,  uwezo  wa kupokea kontena za mizigo utakuwa kati ya kontena 4,000 hadi 6,000.

"Kutakuwa na uwezo wa meli kubwa kuingia, nimewaagiza TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania) warahakishe vifaa kwa ajili ya kupakulia mizigo kwa sababu ufanisi hauwezi kuwepo tena,"  amesema Kamwelwe.

Kwa mujibu wa TPA, ghati hiyo iliyokamilika ujenzi wake Novemba, 2018  ni sehemu ya ghati nane zitakazojengwa kwa Sh968bilioni za mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Uingereza.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz