Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unido yaishauri Serikali kuandaa sera thabiti

20873 Unido+pic TanzaniaWeb

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia viwanda (Unido), Dk Stephen Kargbo amesema Serikali inatakiwa kuandaa sera thabiti ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Hayo ameyasema leo usiku Oktoba 4, 2018 katika Jukwaa la Fikra la Mwananchi linalolenga kujadili fursa, changamoto na ufumbuzi kuelekea uchumi wa viwanda ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na kurushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV.

Amesema sera nzuri zinaweza kuwavutia wawekezaji wengi kuwekeza fedha zao, kuingia ubia mbalimbali na mashirika ili kuongeza mapato katika uchumi wa nchi.

"Sekta binafsi imekuwa ikilalamika mara nyingi katika vyombo vya habari juu ya uharikishwaji wa utekelezaji wa uandaaji sera mbalimbali, hiyo siyo kwa ajili yao tu bali kwa uchumi kwa ujumla," amesema Dk Kargbo na kuongeza:

"Kufanya hivyo kunawafanya wawekezaji kuwa na uhakika wa kesho kulingana na fedha walizowekeza."

Hata hivyo, Dk Kargbo Serikali na sekta binafsi zinapaswa kushikamana ili kuhakikisha ndoto zinakuwa kweli.

"Sio Serikali wala sekta binafsi, kila upande hauwezi kutembea peke yake bali kwa kushikamana" amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz