Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unayotakiwa kuyafahamu kuhusu uwekezaji wa nishati nchini

Nishati Ya Jua Juaaa Unayotakiwa lkuyafahamu kuhu uwekezaji wa nishati nchini

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imesema itahakikisha inaweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya nishati ili kuchochea maendeleo ya uchumi.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ametoa hakikisho hilo leo Oktoba 05, 2023 katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa ushirikiano kwenye sekta hiyo kati ya Tanzania na Uswidi ‘Sweden’ kwa miaka 60.

Pamoja na mambo mengine amesema kuwa Sweden imekuwa na mchango mkubwa katika kuisaidia Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya nishati hususani ya umeme.

"Sweden ni moja ya nchi muhimu inayochangia kwa kiasi kikubwa kwenye miradi ya nishati hususani umeme,” amesema Biteko.

Amesema, Sweden imechangia Sh bilioni 142 kwenye miradi ya ujazilizi katika vitongoji 1328 na Sh bilioni 52 kwa vijiji 151.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live