Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unalijua zao la mwani? hizi ndizo fursa zake..

Algas Mar Unalijua zao la mwani? hizi ndizo fursa zake..

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia wakulima wa zao la Mwani kutoa kilio chao juu ya bei kuwa ndogo na mnunuzi kuwa mmoja huku akipanga bei kwa miaka 17 sasa wamepata wanunuzi zaidi ya watatu.

Mwani ina uwezo wa kutengeneza bidhaa mbalimbali sabuni, mafuta, visheti juice soda mapambo dawa pia chakula kama tukiweza kuiambia jamii tunaweza kuwa na soko kubwa zaidi na kuongeza uzalishaji zaidi.

Tukae Magongo, mkulima wa zao la mwani kutoka katika kijiji cha Mnazi kata ya Nalingu alisema wamekuwa kifungoni kwa miaka 17 ambapo mnunuzi alikuwa mmoja na anapanga bei yake. Also Read

“Biashara ilianzia Sh500 mpaka 1000-1300 na sasa Sh2,000 hii inatunufaisha kwa kuwa hata ukiwa na kidogo unauza unapata pesa hali ya soko sio mbaya, tunao wanunuzi watatu sio sawa na mmoja aliyekuwa akinunua hapo awali,” amesema

Nae Shakifu Kambwili Mkazi wa Kijiji cha Mnazi alisema anashawishika kuanza kulima zao hilo kwakuwa sasa anaona hata mkulima akiwa na kilo mbili anapima na kupata pesa sio kumsubiri boss aje.

Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Mnazi, Faume Mchinji alisema kupanda kwa bei ya mwani ni msaada mkubwa kwa wakulima wa zaod hilo ambapo saasa watapata pesa na kununua vifaa vinavyofaa vinvyotumika kwenye zao hilo.

Nae Mustapha Kwiyunga, Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la Mtwara Society Against Poverty (Msoapo) alisema mpaka sasa vipo vikundi 30 vinavyozalisha zao la mwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

“Awali waliuza mwani mdogo 500 na mwani mkubwa 1000 na mnunuzi alikuwa mmoja tulijitahidi kutangza ambapo sasa tumepata wateja 3 na wanauza kutoka 500-1000 na kutoka 1000 mpaka 2000 mnunuzi alikuwa mmoja kwa miaka 17 na bei alikuwa anapanga yeye.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live