Mbunge wa Tanga Mjini ambaye pia ni Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewawezesha Vijana na Wajasiriamali kwa kuwachangia kiasi Cha zaidi ya Milioni 6 kwa Vikundi mbalimbali Jijini Tanga ukiwa ni Mkakati wa Kuwainua kiuchumi kupitia Ubunifu wa Biashara mbalimbali.
Mhe. Ummy ameeleza kuwa licha ya majukumu ya kitaifa, ataendelea kutimiza wajibu wake kikamilifu wa kuwatumikia wananchi wa Tanga Mjini hususani kutatua kero za maendeleo ya wananchi kupitia fedha za Serikali Kuu, Fedha za Halmashauri pamoja na mshahara wake na posho.
Aidha, katika Kuinua na Kuboresha Mazingira ya Michezo Mhe Mbunge amechangia Shilingi laki 3 kwa ajili ya kukarabati Sehemu ya kufanya mazoezi ya ngumi kwa vijana katika mtaa wa Karafuu, uliopo Jijini Tanga
Wakizungumza baada ya kupokea mchango huo kwa niaba ya vikundi vingine, Ndugu Sadik Ali ambaye ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Nguvu kazi amemshukuru Mhe Mbunge Ummy Mwalimu kwa kuendelea kuwajali wananchi wake katika kuwazesha na Kuwainua kiuchumi na Kuboresha maeneo mbalimbali ya Michezo
Katika ziara hiyo, Mhe Ummy ameongozana na Mhe Habibu Mpa, Diwani wa Kata ya Ngamiani Kati, Mhe Fatuma Kitogo, Diwani wa Viti Maalum pamoja na Viongozi wa CCM ngazi ya Kata na matawi.