Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umeme kupelekwa kwenye migodi mikubwa

Umeme Makutano Umeme kupelekwa kwenye migodi mikubwa

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko amesema Serikali inapeleka umeme katika migodi mikubwa ambayo haikuwa imeunganishwa na umeme akiitaja migodi hiyo kuwa ni pamoja na Geita Gold Mining na Stamigold.

Amesema migodi hiyo kwa miaka mingi ilikuwa ikitumia mafuta kuendesha mitambo yake, hivyo Serikali hivi sasa inakwenda kupumguza gharama za uendeshaji wa migodi hiyo kwa kupeleka umeme.

Dkt. Biteko ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam, alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi rasmi wa Jukwaa la Uwekezaji la Sekta ya Madini Tanzania.

Jukwaa hilo linahudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania pamoja na vikundi mbalimbali ya wachimbaji wa madini na wafanyabiashara wa madini nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live