Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulipaji kodi kwa hiari wapaisha makusanyo

Cdbb7d5d921445f39f03547349ea2351.jpeg Ulipaji kodi kwa hiari wapaisha makusanyo

Sun, 3 Jul 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kutokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya kodi kwa asilimia 99.2 ya lengo la makusanyo ya Sh trilioni 22.5 katika mwaka wa fedha 2021/22, wataalamu wa uchumi wamesema mafanikio hayo ni kutokana na kuwepo kwa mazingira bora ya ulipaji kodi wa hiari.

Wachambuzi wa uchumi walisema hayo kufuatia taarifa ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Alphayo Kidata, iliyotolewa jana ikionesha kwamba katika mwaka wa fedha uliopita, walifanikiwa kukusanya Sh trilioni 22.3 sawa na asilimia 99.2 ya lengo la kukusanya Sh trilioni 22.5.

Katika taarifa hiyo, Kidata pia alitaja mwenendo wa ulipaji kodi kwa hiari kuwa moja ya sababu iliyo- pandisha makusanyo.

Katika mahojiano na gazeti la Habari Leo, mchambuzi wa masuala ya uchumi, Gabriel Mwang’onda, alisema makusanyo na ukuaji wa uchumi ni vitu viwili tofauti kwa kuwa uchumi unakua kwa asilimia ndogo na makusanyo yanakua kwa asilimia kubwa.

“Ili kodi ilipike kwa urahisi lazima iwe na sifa, na moja ya sifa ni kwamba lazima nguvu ya kuikusan- ya iwe ndogo kuliko kiasi kinachokusanywa.

Kwa mfano, kuikusanya kodi ya Sh 20,000 ya wamachinga utatumia nguvu kubwa na haikusanyiki, utatumia gharama kubwa kwa kutumia magari ya halmashauri na kutoa vitambulisho, kodi kama hizi hazitakiwi,” alisema Mwang’onda.

Alisema kodi iliyoboreshwa kama ile ya kukusanya ushuru wa barabara kwa kuiweka kwenye mafuta badala ya kutumia askari, inaweza kuwa moja ya sababu ya makusanyo ku- panda pamoja na matumizi ya namba ya malipo (control number).

Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Humphrey Moshi, alisema kupanda kwa makusanyo hayo kunaweza kuwe kumetokana na TRA kupanua wigo wa kuku- sanya kodi kwa kuwaingiza walipakodi wapya, mwitikio wa wafanyabiashara kutoa risiti na wateja kudai risiti.

Pia alisema kuna haja kwa TRA kupanua zaidi wigo wa kodi kwa kuziingi- za pikipiki ambao wanawe- za kulipa kiasi kidogo na kikawa na tija kwa Taifa.

Katika taarifa yake, Kidata alisema makusanyo hayo ni ongezeko la Sh trilioni 4.1 ikilinganishwa na Sh trilioni 18.2 zilizokusanywa kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha 2020/21.

Alisema ongezeko hilo ni sawa na ukuaji wa makusanyo kwa asilimia 22.8. Alisema katika robo ya nne ya mwaka uliopita, TRA ilikusanya Sh trilioni 5.6 katika lengo la kukusanya Sh trilioni 5.3 ikiwa ni ufanisi wa asilimia 105.5.

Aliongeza kuwa makusanyo hayo ni ukuaji wa asilimia 22.7 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2020/21.

Kwa mujibu wa Kidata, mwezi uliopita, TRA iliku- sanya Sh trilioni 2.3 kati ya lengo la kukusanya Sh tril- ioni 2.1 ikiwa ni ufanisi wa asilimia 113.2 na kuongeza kuwa makusanyo hayo ya mwezi uliopita ni ukuaji wa asilimia 24.8 ikilinganishwa na makusanyo ya mwezi Juni mwaka jana.

“Ufanisi huu ni matokeo ya kuendelea kuimarika kwa matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika usimamizi na ukusanyaji wa kodi, mazingira ya ufanyaji biashara nchini na mwenendo wa ulipaji kodi kwa hiari,” alisema.

Alitaja sababu zingine kuwa ni uboreshwaji wa mahusiano baina ya TRA na walipakodi, utatuzi wa migogoro ya kodi nje ya mahakama, kuongezeka kwa kiwango cha uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa mlipakodi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz