Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulega awataka wadau kuwekeza sekta ya uvuvi

Ulega Pic Data Ulega akizungumza na wadau mjini Kigoma

Mon, 9 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imewataka wadau mbalimbali kuwekeza katika sekta ya uvuvi hasa katika ziwa Tanganyika kwakuwa na teknolojia ya kisasa ya kukausha mazao ya uvuvi hasa dagaa, hatua itakayosaidia kupunguza upotevu wa mazao hayo hasa kipindi cha mvua.

 Akizungumza wakati wa sherehe ya miaka kumi ya mafanikio ya mradi wa Tuungane, unaotekelezwa na mashirika ya kimataifa ya Tanzania Nature Conservancy na PathFinder Internation kwenye vijiji vya kusini vya mwambao mwa Ziwa Tanganyika, Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema sekta ya uvuvi nchini inakabiliwa na changamoto kubwa ya upotevu wa mazao ya uvuvi  hususani dagaa.

Amesema kama watatumia teknolojia hiyo ambazo ni rahisi zitawawezesha kukabiliana na changamoto ya upotevu wa mazao hayo na kwamba wachakataji wa mazao hayo wataona faida endepo hatua hiyo itafanyika.

“Bado kunatatizo kubwa la upotevu wa mazao ya uvuvi hasa katika kipindi cha mvua katika ziwa Tanganyika mmejitahidi kujenga vichanja vya kuanikia na kukausha mazao hayo lakini bado tatizo ni kubwa,”amesema Ulega. 

Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Nature Conservancy (TNC), Lucy Magembe amesema katika kipindi cha miaka 10 kupitia mradi wa Tuungane, wamehifadhi maeneo ya mazalia ya samaki nay a uvuvi yenye ukubwa wa hekta 12,015 katika wilaya ya Uvinza mkoa wa Kigoma na Mlele mkoa wa Katavi.

Mkuu wa wilaya ya Uvinza, Hanaf Msabaha amesema utekelezaji wa mradi wa Tuungane katika wilaya yake umepunguza uvuvi haramu kwa kutoa elimu kwa wavuvi na wachakataji wa mazao ya uvuvi ambao wameweza kufanya dagaa wa kigoma kuwa na thamani.

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live