Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulega akutana na Mkurugenzi Mkuu wa World Fish Dubai

Ulega Akutana Na Mkurugenzi Mkuu Wa World Fish Dubai Ulega akutana na Mkurugenzi Mkuu wa World Fish Dubai

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa WorldFish, Dkt. Essam Yassin Mohammed pembezoni mwa Mkutano wa COP 28, Dubai, UAE.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika leo Disemba 4, 2023, Mhe. Ulega amemweleza Mkurugenzi huyo kuhusu nia ya Tanzania ya kutaka kushirikiana na WorldFish katika kuimarisha Sekta ya Uvuvi ili iwe na mchango mkubwa zaidi kwa Taifa.

Aidha, pamoja mambo mengine, wamekubaliana kuhakikisha kwamba Taasisi hiyo inaweka nguvu katika afua za kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo uoteshaji wa matumbawe, kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi baada ya kuvunwa, kukuza ukuzaji viumbe maji bahari na kuboresha kosaafu za viumbe maji wakuzwao huku akimkaribisha kufungua ofisi ya WordFish nchini Tanzania.

WorldFish ni taasisi ya kimataifa kutoka nchini Malaysia ambayo inashughulika na utafiti na ubunifu katika minyororo ya thamani ya uvuvi na ukuzaji viumbe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live