Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulega ahimiza kilimo cha malisho

ULEGA JUNI 2019 Ulega ahimiza kilimo cha malisho

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameendelea kuwahimiza wafugaji kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya kulima malisho ili kuwa na uhakika wa malisho kwa ajili ya mifugo yao wakati wote.

Waziri Ulega ametoa wito huo alipotembelea shamba la mbegu na malisho la wizara hiyo lililopo Vikuge, Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani, Disemba 13, 2023. Shamba hilo ni miongoni mwa mashamba ya malisho ya mifugo ambayo Serikali imefanya uwekezaji mkubwa.

Wakati akikabidhi mbegu za malisho za aina ya Juncao kwa baadhi ya wafugaji waliofika shambani hapo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wafugaji kuona umuhimu wa kulima malisho, Waziri Ulega alisema kuwa kila mfugaji ni muhimu awe na eneo la malisho kwani itawasaidia kuondokana na migogoro baina yao na wakulima.

Naye, Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Dkt. Asimwe Rwiguza amesema kuwa mbegu hizo za Juncao zilizopo katika shamba la Vikuge litasaidia kupunguza changamoto ya malisho huku akisema kuwa mpango wa Wizara ni kusambaza mbegu za malisho hayo katika mashamba mengine ya Wizara yaliyopo mikoani ili kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live