Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulega: Tutauza tani elfu 50 za nyama nje ya nchi

Nyama Za Ng'ombe Ulega: Tutauza tani elfu 50 za nyama nje ya nchi

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeiwezesha Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kiasi cha shilingi bilioni 4.65 kwa ajili ya kununua vitendea kazi na ng'ombe wazazi ili kuboresha na kuongeza uzalishaji wa kampuni hiyo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega aliyoifanya katika Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma wakati akizindua matreka mapya matano (5) na kupokea ngo'mbe elfu moja (1000) kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa kampuni ya NARCO.

"Hivi sasa tumeshafika katika kiwango cha kuuza nje ya nchi nyama tani elfu 12, na kuanzia mwaka ujao na kuendelea tutatoka kwenye tani elfu 12 na kutafuta tani elfu 50 na ikiwezekana mpaka tani laki moja", amesema Waziri Ulega

Ameendelea kusema kuwa katika mkakati wa kuifufua kampuni ya NARCO pia wataanzisha skimu za unenepeshaji wa mifugo ili nyama itakayokuwa inazalishwa kutoka NARCO iwe na ubora wa kuiuza nje ya nchi.

"Tunakusudia kwamba mchango wa sekta ya mifugo uongezeke kutoka asilimia 7 hadi kufikia asilimia zaidi ya 10, na hilo linawezekana kwa sababu rasilimali ya kutuwezesha kufikia huko tunayo", alisisitiza

Aidha, amesema kuwa serikali ina mipango ya kuanzisha skimu za umwagiliaji wa malisho ili yaweze kuzalisha kwa wingi kwa ajili ya kuyauza ndani na nje ya nchi.

"Kama ambavyo huwa tunasafirisha mahindi kutoka maeneo mbalimbali na kuwapelekea wahitaji tunataka pia tuzalishe malisho kwa wingi na kuyasafirisha kuyapeleka kwa wahitaji waliopo ndani na nje ya nchi", alifafanua

Chanzo: www.tanzaniaweb.live