Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulega: Mchango wa sekta ya Mifugo na Uvuvi upo chini

ULEGA JUNI 2019 Ulega : Mchango wa sekta ya Mifugo na Uvuvi upo chini

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewataka Wataalam wa sekta za Mifugo na Uvuvi nchini kuongeza ubunifu katika shughuli zao ili mchango wa sekta hizo katika uchumi wa Taifa uweze kuongezeka tofauti na ilivyo sasa ambapo sekta ya uvuvi inachangia asilimia 1. 8 na sekta ya mifugo inachangia asilimia 7.0.

Waziri Ulega ameyasema hayo mkoani Arusha wakati akifungua Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP).

Amewataka Wataalam hao kuendeleza sekta hizo kwani huu ni wakati mwafaka wa kufanya mapinduzi makubwa katika minyororo ya thamani ya mifugo na mazao ya samaki nchini.

Naye Mwenyekiti wa TSAP Dkt. Jonas Kizima amesema moja ya malengo ya chama hicho ni kuhimiza maendeleo katika sayansi ya uzalishaji wa mifugo na uvuvi nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live