Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulega: Lengo ni kugawa boti 500 za uvuvi

Ulega Msgs Ulega: Lengo ni kugawa boti 500 za uvuvi

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema katika mwaka wa fedha wa 2024/2025 wizara hiyo imepanga kuongeza idadi ya boti za kisasa kwa wavuvi kutoka 160 na kugawa boti 500 zaidi ili kuwawezesha wavuvi kote nchini kufanya shughuli zao kisasa.

Akitoa maelezo mkoani Mwanza kuhusu mradi wa kugawa boti na vizimba vya ufugaji wa samaki kwa Kanda ya Ziwa waziri Ulega amesema, mpango uliopo kwa mwaka ujao wa fedha ni kugawa boti 500 kwenye maeneo mbalimbali nchini ili mradi huo uwe na tija.

Amesema boti zilizogawiwa leo ni sehemu ya boti 160 zilizonunuliwa na Serikali katika mpango wa awali na ili kuuendeleza wizara ya Mifugo na Uvuvi itafanya jitihada kupata boti zaidi za kuwawezesha wavuvi wadogo.

Mradi huo ambao umehusisha pia vizimba 222 vya kufugia samaki, utawanufaisha Wananchi takribani 980.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live