Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulega: Chato kuna fursa nyingi za uwekezaji

Ulega Ulega: Chato kuna fursa nyingi za uwekezaji

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amefungua Tamasha la Utalii wilayani Chato mkoani Geita "Chato Utalii Festival 2023" linalofanyika kwa lengo la kuhamasisha shughuli za utalii na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo wilayani humo.

Akizungumza wakati akifungua tamasha hilo ambalo linafanyika kwa pamoja na maonesho mbalimbali ya fursa zilizopo mkoani Geita, Waziri Ulega amesema tamasha hilo limebeba dhana mbalimbali za uwekezaji hasa kwa upande wa kilimo, mifugo na uvuvi, utalii, utamaduni na michezo.

Amesema fursa za uwekezaji zilizopo wilayani Chato ni nyingi na amewahimiza Wananchi na wawekezaji mbalimbali kuzitumia ili ziweze kuwaletea ufanisi na kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja.

Kwa upande wa sekta ya mifugo, Waziri Ulega amesema wamejenga mnada wa mifugo wa kisasa wa Buzirayombo ambao unatoa fursa kwa wafugaji kufanya biashara zao za mifugo kisasa na kunatoa fursa nyingine ya kujenga kiwanda cha kuchakata nyama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live