Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulega: Changamkieni biashara ya majongoo bahari, mwani

Mwani Mwani Ulega: Changamkieni biashara ya majongoo bahari, mwani

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewahimiza wakazi wa Mtwara na maeneo mengine ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi kuchangamkia fursa ya ufugaji wa majongoo bahari, kaa, kambakochi na kilimo cha Mwani kwa sababu mazao hayo yana soko kubwa katika nchi za Asia hususan China.

Waziri Ulega ametoa rai hiyo jana Jumapili, Januari 14, 2024 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Ukuzaji Viumbe Maji cha Ruvula kinachojengwa Msimbati, mkoani Mtwara.

“Mahitaji ya majongoo bahari, kaa, mwani, kambakochi na mwatiko ni makubwa katika nchi za Asia hasa China, hivyo ni lazima tucheze na fursa tulizonazo ili tuweze kufanikiwa na ndio maana Serikali inatoa elimu kuwawezesha wananchi hususan vijana na kinamama kufanya shughuli hizo ili wauze nje ya nchi wajipatie kipato”, amesema Ulega

Pia amewahimiza wananchi kujipanga vyema ikiwemo kuunda vikundi ili Serikali iatambue na kuwapatia mikopo ya vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi mkubwa.

Waziri Ulega ameonyesha kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha ukuzaji viumbe maji cha Ruvula huku akiamini kuwa kitakamilika kwa wakati ili kianze kufanya kazi.

Awali, Mhandisi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, George Kwandu alimweleza Waziri Ulega kuwa ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 90 na itakapofika Januari 30, 2024 mradi huo utakuwa umekamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live