Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukuaji uchumi Tanzania kufikia asilimia 6.1 mwakani

Profesa Kitila Mkumbo.jpeg Ukuaji uchumi Tanzania kufikia asilimia 6.1 mwakani

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema Pamoja na changamoto zilizotokana na athari za ugonjwa wa UVIKO 19 na vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine, viashiria vya uchumi wa Tanzania vimeendelea kuwa tulivu ambapo kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2022 kilikuwa asilimia 4.7 na kinatarajiwa kufikia asilimia 5.2 mwaka 2023 na asilimia 6.1 mwaka 2024.

Prof. Mkumbo amesema hayo wakati akianisha mafanikio 10 yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2022/2023 na robo ya kwanza ya Mpango wa Mwaka 2023/2024 wakati akiwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2024/2025 leo November 06,2023.

“Pamoja na changamoto zilizotokana na athari za ugonjwa wa UVIKO 19 na vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine, viashiria vya uchumi wa Nchi yetu vimeendelea kuwa tulivu, kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2022 kilikuwa asilimia 4.7 na kinatarajiwa kufikia asilimia 5.2 mwaka 2023 na asilimia 6.1 mwaka 2024”

“Mfumuko wa bei uliendelea kuwa tulivu ambapo ulikuwa asilimia 4.3 kwa mwaka 2022 na ulipungua na kufikia asilimia 3.3 katika kipindi kilichoishia September 2023”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live