Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukosefu wa umeme kikwazo kwa wachimbaji wadogo Chunya

Misri Yatangaza Mgao Wa Umeme Kutokana Na Joto Kali Ukosefu wa umeme kikwazo kwa wachimbaji wadogo Chunya

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya wamesema ukosefu wa nishati ya umeme wa uhakika ni kikwazo kikubwa katika uendeshaji wa shughuli za kila siku na kujikuta wakitumia gharama kubwa za kununua mafuta ya dizeli.

Hali hiyo imeelezwa kuwa ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha kufikia malengo ya kiuchumi kutokana na idadi kubwa ya vijana kujihusha zaidi kwenye uchimbaji wa madini.

Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Kampuni ya AGM Mpangwe, Andrew Mpangwe ameliambia Mwananchi Digital leo Jumatatu Oktoba 30, 2023 na kwamba kwa sasa katika Wilaya ya Chunya kumekuwa na changamoto ya umeme kukatika asubuhi na kurejea jioni au baada ya masaa kadhaa.

“Kimsingi hili suala ni changamoto kubwa ambayo tunashindwa kuendesha maisha yetu ya kila siku na hata namna ya kuwalipa vijana tunao waajiri tunaomba Serikali kuangalia njia mbadala ya kunusuru na janga hili,”amesema.

Amesema kuwa kutokana na adha hiyo amejikuta kwa siku akitumia zaidi ya Sh100,000 mpaka Sh150,000 kununua mafuta ya dizeli kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake, wakati umeme ungekuwepo alikuwa akitumia Sh10,000 mpaka 20,000 kwa siku,” amesema.

Amesema kuwa ufike wakati Serikali ikaangalia njia mbadala ya kuzalisha nishati ya umeme kwa kuzingatia halmashauri ya Wilaya ya Chunya kutegemea mapato yake kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu.

Mpangwe ameongeza kuwa kukosekana kwa mapato ya Serikali pia kutakwamisha kushindwa kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo hususan katika sekta ya elimu, maji na miundombinu.

Aidha katika hatua nyingine, Mpangwe ameomba Serikali na Taasisi za kifedha kuunga mkono jitihada zao za uzalishaji mali kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ili waweze kupiga hatua za kiuchumi.

“Mimi mbali na kuwekeza kwenye shughuli za uchimbaji wa madini pia na katakana ya kuchonga makarasha na vifaa vinavyotumika migodini lakini kuna changamoto ya uendeshaji hususan mitaji isiyolingana na mahitaji ya bidhaa,”amesema.

Mustapha Ramadhan amesema kuwa ukosefu wa umeme wa uhakika unachangia uchumi wao kuporomoka na kuomba Serikali kutafua njia mbadala ya kuondoa tatizo la umeme.

“Kitendo cha umeme kukatika kutoa asubuhi mpaka jioni ni changamoto kubwa ya uendeshaji wa shughuli zetu ikiwepo kuchomelea na hata kwenye machimbo hali ambayo inasababisha ndoa kuwa na migogoro kutokana na ukosefu wa kipato,” amesema.

Mfanyabishara wa vinywaji baridi, Salome Joel amesema kwa sasa biashara imekuwa haitabiriki kwani Wilaya ya Chunya kuna jua kali linalosababisha joto huku idadi kubwa ya wateja kuhitaji vinywaji baridi.

“Awali mauzo kwa siku ilikuwa kati ya Sh 250,000 mpaka 300,000 lakini sasa yameporomoka mpaka 150,000 jambo ambalo ni changamoto kubwa ya uendeshaji, ulipaji wa pango la nyumba na wafanyakazi,”amesema.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka amekiri kuwepo kwa changamoto ya kukatika kwa umeme na kwamba tayari Serikali iko kwenye mpango wa kujenga kituo cha kusambaza umeme ambao utatoka kwenye mradi mkubwa wa bwawa la Mwalimu Nyerere.

“Umeme ni changamoto sana hususan kwa maeneo ya wachimbaji wadogo wa madini lakini tuna imani kupitia ujenzi wa kituo hicho itakuwa mwarobaini wa tatizo,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live