Soko kuu la Manispaa ya Shinyanga lililojengwa zaidi ya miaka 40 iliyopita na kusababisha miundombinu yake kuchakaa, limeanza kufanyiwa ukarabati kwa kujenga gorofa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika mazingira mazuri na salama
Akizungumza na wafanyabishara Mstahikimeya Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amewataka kuendelea kulipa ushuru wa huduma pamaoja na kulipia leseni zao, kutokana na fedha hizo kuwanufaisha wananchi kwa kuboresha miundombinu, badala ya kuishia mifukoni kwa watu wachache kwa maslahi yao binafsi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wa viwanda na kilimo (TCCIA)Mkoa wa Shinyanga Dk. Kulwa Meshack, amesema wataendelea kusimamia ili ujenzi ukamilike mapema, huku msimamizi wa ujenzi Snatus Kuchibanda amesema ujenzi utafanyika usiku na mchana
Nao baadhi ya wafanyabiashara wa soko kuu, wamesema ujenzi huo utasaidia kuboresha miundombinu iliyopo.