Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukarabati wafikia asilimia 80 kivuko MV KAZI

MV Ukarabati wafikia asilimia 80 kivuko MV KAZI

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukarabati wa kivuko cha MV. KAZI kinachofanya safari zake kati ya Magogoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam umekamilika kwa asilimia 80 ambapo mwezi ujao kinatarajiwa kurejea kuanza kutoa huduma.

Kivuko hicho kiliondolewa rasmi kwenye maji mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu baada yakufikia muda wake wa ukarabati ambapo ni miaka mitatu hadi mitano tangu kianze kutoa huduma.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro Kilahala mwishoni mwa wiki hii wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Yadi ya Songoro Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo kivuko hicho kinaendelea kufanyiwa ukarabati.

"Tumefanya ukaguzi wa mwisho takribani mwezi mmoja uliopita, kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ilikuwa ni vifaa, kwa sababu ile kazi sehemu kubwa ilikuwa ni kufunga vifaa vipya vya injini, gia boksi, na mifumo mipya ya injini, kwa hiyo zile kazi ambazo zilikuwa zinaweza kufanyika kabla ya vifaa hivyo ilikuwa zaidi ya asilimia themanini na zote zilifanyika ikiwemo kazi za kuondoa vipande vya bati ambavyo vimeharibika na kupiga rangi upya," alisema Mtendaji Mkuu.

Awali, Mwakilishi wa kampuni ya Songoro Marine wanaofanya ukarabati wa kivuko hicho Hamad Aweso akizungumza na waandishi wa habari amesema ukarabati wa kivuko hicho umefikia hatua nzuri na amebainisha kuwa kuna vifaa ambavyo vilichelewa kufika kwa wakati zikiwemo injini za kivuko hicho na kwa sasa vifaa hivyo vimeshafika hivyo kazi iliyobaki ni kuvifunga ili kivuko kiweze kurejea kutoa huduma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live