Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujumbe wa Samia kwa mabenki nchini Tanzania

62718 Makamupic

Sat, 15 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameyataka mabenki nchini Tanzania kuzingatia mambo matatu ili kujiendesha kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kutojiingiza katika kashfa ya mtandao wa kutakatisha fedha.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 14, 2019 katika uzinduzi wa tawi la benki ya biashara Mkombozi jijini Dodoma huku akiitaka benki hiyo kuweka riba ya mikopo inayoendana na maisha halisi ya Watanzania.

“Epukeni kuiingiza benki katika kashfa na mitandao ya kutakatisha fedha kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za kifedha na sheria nyingine.”

“Himizeni matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao kuokoa muda, gharama na usalama zaidi na mhakikishe mnaboresha huduma zenu ziwafikie wananchi wote, hasa wa kipato cha chini pale walipo kwa haraka  na nafuu. Mfike hadi vijijini msibaki mjini pekee,” amesema Samia.

Kuhusu riba ya asilimia 2.5 kwa mwezi kwa wajasiriamali wadogo inayotolewa na benki hiyo, Samia amesema ingawa ni ndogo lakini kwa mwaka ni sawa na asilimia 30, kuomba jambo hilo kufanyiwa kazi ili kuwe na riba itakayowanufaisha zaidi wananchi.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz