Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujerumani yaipa Tanzania Sh5.2 bilioni kulinda Bahari ya Hindi

Hahari Pic Data Ujerumani yaipa Tanzania Sh5.2 bilioni kulinda Bahari ya Hindi

Sun, 15 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Rashid Tamatamah amesema Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) litaipatia Tanzania Sh 5.2 bilioni kwa ajili ya mradi wa Uhifadhi wa Bainuai za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani.

Taarifa ilitolewa kwa vyombo vya habari na leo Jumapili Mei 15, 2022 na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imeeleza imesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya ujumbe wa ubalozi wa Ujerumani nchini na uongozi wa GIZ kufanya mazungumzo na Dk Tamatamah anayeshughulikia sekta ya uvuvi.

Dk Tamatamah amesema katika Ukanda wa Bahari ya Hindi kutakuwa na miradi mingi na kuanzia Agosti mwaka huu mradi huo utaanza kufanyika Kaskazini mwa Tanzania katika wilayani Mkinga mkoani Tanga.

“Huu mradi una faida unalenga kuhifadhi bainuai, utatoa elimu kwa jamii inayokaa katika maeneo hayo na tunategemea utafanya rasilimali kuwa endelevu kwa muda mrefu na utaongeza kipato kwa wananchi.

“Kupitia mradi huu wananchi wataelimishwa njia mbadala za maisha na kuhifadhi maeneo tengefu,” amesema Dk Tamatamah.

Katika mazungumzo hayo, Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani, Dk Katrin Bornemann na Mratibu wa GIZ, nchini Ralf Senzel wamesema wataipatia Tanzania ili kutekeleza mradi huo, kwa miaka minne.

Dk Bornemann amesema  wana furaha kuona ushirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania katika maeneo ya bainuani na maeneo tengefu utakuwa na nguvu ili kuhakikisha ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi unatunzwa na  rasilimali zilizopo maeneo hayo zinaendelezwa.

Kwa upande wake, Senzel amesema, “mradi huo utajenga uhusiano mzuri baina ya Ujerumani na Tanzania,” amesema.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (Tafiri), Dk Ismael Kimirei, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) John Komakoma.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mradi huo utatekelezwa na Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish), Nichrous Mlalila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live