Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi wa daraja Tanzania, Msumbuji mbioni kuanza

Waziri Wa Ujenzi, Innocent Bashungwa Ujenzi wa daraja Tanzania, Msumbuji mbioni kuanza

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho ya kusiani mkataba na kumtangaza Mkandarasi atayejenga barabara ya Likuyufusi - Mkenda (km 122) sehemu ya kwanza Likuyufusi - Mkayukayu (km 60) kwa kiwango cha lami kwa ajili ya kurahisisha biashara ya mazao kati ya Tanzania na Msumbiji.

Ujenzi wa barabara hiyo utaenda sambamba na ujenzi wa Daraja la Kisasa la Zege mpakani mwa Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji eneo la Mkenda Wilayani Songea kwa ajili ya kuufungua Mkoa wa Ruvuma kiuchumi.

Bashungwa ameeleza hayo wilayani Songea wakati akikagua barabara pamoja na Daraja la chuma la muda la Mkenda katika Mto Ruvuma.

“Kujengwa kwa barabara hii kutawasaidia wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ambao ni wazalishaji wakubwa wa mazao na utainua uchumi wa Nchi yetu kuweza kusafirisha kutoka Tanzania kwenda nchi jirani ya Msumbiji”, amesema Bashungwa.

Akitoa taarifa ya mradi, Mkurugenzi wa Miradi kutoka TANROADS, Mhandisi Jephason Nko ameeleza kuwa ujenzi wa barabara hiyo utahusisha ujenzi wa madaraja makubwa mawili, madaraja madogo pamoja na makalvati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live