Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi wa bomba la mafuta Uganda hadi Tanzania wafadhiri wajitoa

Mafuta Mn.jpeg Bomba la mafuta

Sat, 21 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Deutsche imeripotiwa kwamba haitafadhili mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoina Uganda hadi Tanga, Tanzania.

Hii ni baada ya wanaharakati wa mazingira kuasilisha malalamishi kwamba ujenzi wa bomba hilo utapelekea watu kadhaa kukoseshwa makao, pamoja na kuvuruga maisha ya wanyama wa porini.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba benki hiyo kubwa ya Ujerumani imekumbana na shinkizo kubwa kutaka kueleza mkataba wake wa ufadhili wa mradi huo wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta, utakaogharimu kiasi cha dola bilioni 3.5.

Bomba hilo lina urefu wa kilomita 1,400, kati ya Uganda na Tanzania. Benki ya Deutsche haijatoa taarifa kamili lakini kundi la kutetea mazingira la 350.org linapanga maandamano kupinga ufadhili wake katika siku zijazo.

Kundi hilo limesema kwamba wafadhili kadhaa wa mradi huo na mashirika ya bima yamejiondoa na sasa wanataka benki ya Deutsche kujiondoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live