Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi uwanja wa ndege Musoma wafikia asilimia 55

Uwanja Wa Ndege Musoma Ujenzi uwanja wa ndege Musoma wafikia asilimia 55

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Musoma uliopo mkoani Mara ambapo amesema ni faraja kuona Serikali ikiendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati ukiwemo uwanja huo.

Amesema uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kutoa fedha kwa ajili ya upanuzi wa uwanja huo ni ya kuungwa mkono kwa kuwa ni fursa kwa Wafanyabiashara na wakazi wa maeneo hayo.

“Uwanja huu utaleta fursa kwa Wafanyabiashara na wakazi wa mkoa huu na wilaya zake kwa sababu utawezesha kuendelea kukua kwa sekta ya utalii kwenye mkoa huu ambao kuna mbuga ya Serengeti,” Amesema Waziri Mkuu.

Ujenzi wa uwanja huo wa ndege wa Musoma ambao umefikia asilimia 55 utagharimu shilingi Bilioni 35 na utahusiaha ukarabati wa njia ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa mita 1,705 na upana mita 30 kwa kiwango cha lami, ukarabati wa njia ya kiungio kwa kiwango cha lami na ukarabati wa eneo la maegesho ya ndege kwa kiwango cha lami.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live