Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi uwanja wa ndege Iringa wafikia asilimia 82

Uwanja Wa Ndege Iringa.png Ujenzi uwanja wa ndege Iringa wafikia asilimia 82

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Nduli mkoani Iringa, umefikia asilimia 82 na ukitarajiwa kukamilika mwishoni wa Desemba 2023.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, David Kihenzile amesema hayo baada ya kutembelea kiwanja hicho ambacho kimegharimu zaidi ya Sh63.7 bilioni, ili kuangalia maendeleo ya ujenzi wake.

"Ujenzi wa kiwanja hiki cha ndege kitasaidia kuinua uchumi wa wakazi wa mkoa wa Iringa kupitia sekta mbalimbali ikiwemo utalii kwakuwa unaunganisha dunia na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha," amesema Kihenzile

Pia ameeleza Serikali inajenga barabara ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa kiwango cha lami lengo ikiwa ni kufanya utalii unakuwa wa kisasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live