Ujenzi wa kiwanda cha kuwekea mifumo ya upashwaji joto mafuta pamoja na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika kwenye mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) umefikia aslimia 40 katika Kijiji Cha Sojo Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora.
Akizungumza, Mratibu wa mradi huo Asiad Mrutu amesema ujenzi wa karakana umefikia asilimia 90 huku wataalam wakiendelea na ujenzi wa miundombinu mingine kiwandani hapo.
Amesema tayari mabomba ya majaribio yameshafika Sojo, huku mabomba mengine yakitarajiwa kufika mwezi Novemba, 2023 tayari kuanza kutengenezwa na kusambazwa kwenye kambi 14 zilizojengwa nchini kati ya kambi 16 za mradi wote.
Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima - Uganda hadi Chongoleani - Tanga lenye urefu wa kilomita 1,447 utagharimu shilingi Trilioni 11 hadi kukamilika kwake.