Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi kituo cha kupoza umeme mgodini wafikia asilimia 95

Umeme.png Ujenzi kituo cha kupoza umeme mgodini wafikia asilimia 95

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matumaini ya Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kuanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), katika kutekeleza majukumu yake yameanza kuonekana baada ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme unaofikishwa mgodini hapo kufikia asilimia 95.

Kituo hicho kinachojengwa kwa gharama ya Sh60.6 bilioni kitakuwa na uwezo kupooza umeme wa msongo wa kilovoti 33 kuwa kilovolt 11 ndani ya mgodi wa GGML na kina uwezo wa megawati 40.

Akitoa taarifa hivi karibuni kwa Ofisa mkuu wa masuala ya Fedha kutoka AngloGold Ashanti ambayo ni kampuni mama ya GGML, Gillian Doran, Mhandisi mwandamizi anayesimamia ubora na viwango katika miradi ya kampuni hiyo, Maftah Seif amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika katikati ya Machi 2024 kulingana na hali ya upatikanaji wa umeme wa Tanesco.

New Content Item (1)

Amesema kazi kubwa iliyobaki sasa ni kukamilisha ufungaji wa mifumo ya mitambo hiyo na kuanza majaribio.

Awali, akifafanua kuhusu mradi huo, Makamu Rais wa AngloGold Ashanti anayeshughulikia miradi endelevu na masuala ya ubia/ushirika Afrika, Simon Shayo amesema Tanesco wameshakamilisha ujenzi wa laini ya kilovolt 220 kutoka Bulyanhulu hadi Geita huku ujenzi wa laini ya kilomita sita yenye kilovolt 33 kwenda katika mgodi wa GGML ipo katika hatua za mwisho.

Amesema licha ya kampuni nyingi za madini tangu miaka ya 2000 hutumia umeme wanaouzalisha wenyewe, sasa Serikali imekuwa na jitihada za makusudi kufungamanisha sekta ya nishati na sekta kubwa za uzalishaji kwa kuzalisha umeme unaotosheleza mahitaji ya wawekezaji wakubwa.

"Sisi kwa sekta ya madini tunaona hii kama ni baraka kubwa kwa sababu huwezi kuendesha migodi mikubwa kama ya kwetu (GGML) kwa kutumia jenereta," amesema.

Ametolea mfano GGML hutumia megawati 40 ambazo huzalisha kwa mafuta ya dizeli lakini sasa wanatamani kuona mradi wa kupeleka umeme wa Tanesco katika mgodi wa kampuni hiyo ukikamilika ili kupunguza gharama za uendeshaji.

"Tukijiunga tu na Tanesco kwenye gridi ya Taifa na kutoka kwenye umeme tunaouzalisha wenyewe, tutapunguza gharama za umeme kwa asilimia 50, tutaokoa Dola za Marekani milioni 19 kila mwaka. Pia tutapunguza hewa ya ukaa kilotons 81 kufikia 2030," amesema.

Amesema kwa kuwa nchi ipo katika mipango ya kuwekeza zaidi katika sekta ya madini kwa kuanzisha migodi mingine ya uzalishaji madini sehemu mbalimbali nchini, ni dhahiri kuwa Tanesco itafanikiwa kuongeza mapato kutokana na mchango wa sekta hiyo kwenye matumizi ya umeme.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live