Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi daraja la Magufuli wafikia asilimia 78

Kigongo Busisi 16dec19 (600 X 311) Ujenzi daraja la Magufuli wafikia asilimia 78

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MENEJA wa Wakala ya Barabara (TANROADS) mkoani Mwanza, Mhandisi Paschal Ambrose amesema ujenzi wa daraja la Magufuli (Kigongo Busisi) limefikia asilimia 78.

Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 3.2 limejengwa na idadi kubwa ya wakandarasi wazawa kati ya 750 hadi 1000 ambapo wakandarasi kutoka nje ya nchi ni 57 tu.

Mhandisi Ambrose amesema hayo Novemba 7, 2023 alipozungumza na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Shinyanga, Mara, Geita na Mwanza katika ofisi za Tanroads mkoani humo.

"Mradi wa ujenzi wa daraja hilo ulianza mwaka 2020, mwezi February na kipindi cha miaka miwili na nusu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu alikuta ujenzi umefikia asilimia 25 na ameweza kutoa fedha za uendelezaji wa mradi huo wa kimkakati na Sasa umefikia asilimia 78."alisema Mhandisi Ambrose.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live