Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi daraja la JPM wafikia asilimia 74

Daraja JPM JPM (600 X 345) Ujenzi daraja la JPM wafikia asilimia 74

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan, daraja la JP Magufuli limefikia asilimia 74 ya ujenzi wake, ambapo mpaka sasa Sh bilioni 368.671 zimetolewa kwa Mkandarasi China Civil Engineering.

Mkurugenzi wa Miradi na Maendeleo Tanroads, Mhandisi Boniface Mkumbo, amesema wakati Rais Samia ameingia madarakani ujenzi wa daraja hilo ulikuwa asilimia 26 na kiasi ambacho kilitolewa ni Sh bilioni 118.

“Daraja hili litaanza kutumika rasmi Februari 24, 2024,” amesema Mkumbo katika kongamano la miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan linaloendelea mkoani Mwanza. Daraja hilo linaunganisha eneo la Kigongo wilayani Misungwi na Busisi wilayani Sengerema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live