Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi bwawa la Kidunda waiva

Bwawa Kidundaaaaaaa.png Ujenzi bwawa la Kidunda waiva

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Kiula Kingu amesema maandalizi ya mradi wa ujenzi bwawa la Kidunda unaotegemewa kuanza Juni 18 mwaka huu yapo katika hatua nzuri.

Kiula ameyasema hayo wakati wa ziara ya Menejimenti ya Dawasa katika eneo la mradi huo unaojengwa katika Kata ya Kidunda, Halmashauri ya Morogoro Vijijini. Mradi huu ni muhimu katika kutatua changamoto ya upungufu wa maji katika mto Ruvu wakati wa kiangazi.

“Mradi huu ni wa kimkakati utakaowezesha mto Ruvu kuwa na maji ya kutosha mwaka mzima hivyo kuiwezesha Dawasa kutoa huduma stahiki za maji hata kunapotokea kiangazi cha muda mrefu,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live