Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi bandari ya Mbamba Bay waiva...

Mbamba Bay Ujenziii.png Ujenzi bandari ya Mbamba Bay waiva...

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeikabidhi rasmi kampuni ya Anova Consulting Company ltd eneo itakapojengwa Bandari ya Mbamba Bay iliyopo wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Manga Gassaya amesema kampuni hiyo itasimamia ujenzi wa bandari ya Mbamba Bay ili kuhakikisha kila kitu kinafanyika katika viwango na kukamilika kwa muda uliokubaliwa katika mkataba.

Amesema kuwa kinachofanyika ni kumuonesha msimamizi wa mradi (Anova Consult) mipaka ya eneo la ujenzi.

Makabidhiano hayo ni kufuatia mkataba wa usanifu na ujenzi wa uendelezaji wa Bandari ya Mbamba Bay uliosainiwa Desemba 04, 2023 ambapo kampuni ya Xiamen Ongoing Construction Group Co ltd ndio itaendeleza ujenzi wa Bandari hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live