Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi SGR Dar- Morogoro wafikia 97%

9c1d627db13ebd01c27f55fb0b0ae670.jpeg Ujenzi SGR Dar- Morogoro wafikia 97%

Wed, 19 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

UJENZI wa reli ya kisasa (SGR) kwa kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro umefikia asilimia 91.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho alisema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha mpango na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Ujenzi wa reli hiyo inayjengwa na kampuni ya Uturuki ya Yapi Merkezi ulianza Mei mwaka 2017.

Dk Chamuriho aliwaeleza wabunge kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka jana hadi Aprili mwaka huu, serikali imeendelea kusimamia ujenzi wa reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.

“Ujenzi wa reli ya kati kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa kilometa 300 umekamilika kwa asilimia 91. Shughuli zinazoendelea ni pamoja na ujenzi wa makalvati uliokamilika kwa asilimia

99.7, ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 2.5 katikati ya Jiji la Dar es Salaam umekamilika kwa asilimia 94.2 pamoja na kutandika reli

kwenye urefu wa kilometa 257,” alisema.

Alisema kazi ya ujenzi wa vivuko umekamilika kwa asilimia 99 na ujenzi wa stesheni umekamilika kwa asilimia 99.8.

Kuhusu kipande cha reli cha kutoka Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa kilometa 422, alisema ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 60.2.

Dk Chamuriho alisema kazi zinazoendelea kufanyika ni pamoja na usanifu ambao umefikia asilimia 89.1, uzalishaji wa mataruma ya

zege uliofikia asilimia 92.6, kutandika reli kwenye urefu wa kilometa 99, ukataji wa miinuko na ujazaji mabonde uliokamilika kwa asilimia

90.6.

Kazi zingine ni pamoja na uchorongaji wa mahandaki manne uliokamilika kwa asilimia 100, ujenzi wa makalvati uliofikia asilimia 75.1, ujenzi wa vivuko vya mifugo uliofikia asilimia 83.3 na ujenzi wa stesheni uliofikia asilimia 50.1.

“Kazi za ujenzi wa mfumo wa umeme katika mradi wa SGR imekamilika kwa asilimia 100 kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na asilimia 35.6 kwa kipande cha Morogoro hadi Makutupora,” alisema Dk Chamuriho.

Kwa mujibu wa Dk Chamuriho, Januari 8 mwaka huu, serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) ilisaini mkataba wa ubia na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) na China Railways Construction Cooperation (CRCC) za nchini China kwa ajili ya ujenzi wa reli ya SGR kutoka Mwanza hadi Isaka yenye urefu wa kilometa 341.

“Malipo ya awali ya ujenzi wa kipande hiki ya shilingi bilioni 376.4 yamefanyika Aprili mwaka huu. Kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu na sasa Mkandarasi anaendelea na maandalizi ya ujenzi ikiwemo uletaji wa mitambo,” alisema Dk Chamuriho.

Kuhusu ujenzi wa reli hiyo kwa vipande vya Makutupora–Tabora chenye urefu wa kilometa 294 na Tabora–Isaka chenye urefu wa kilometa 133, alisema serikali inaendelea na majadiliano na Taasisi za fedha na Washirika mbalimnali wa Maendeleo walioonesha nia ya kugharamia ujenzi huo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz