Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhaba wa mayai waikumba New Zealand

Mayai Kenya Uganda Mayai

Sat, 14 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

New Zealand yakabiliwa na uhaba wa mayai nchini kote jambo ambalo limesababisaha bei ya jumla kupanda na kupelekea chakula aina ya dessert na pavlova vinavyopendwa nchini humo kuwa hatarini.

Maduka makubwa safu zake zipo wazi bila mayai na baadhi ya maduka yanaweka vikwazo kwa idadi ya mayai ambayo wateja wanaweza kununua.

Marufuku ya serikali iliyosubiriwa kwa muda mrefu ya kuzuia kuku waliofungiwa na betri ilianza kutekelezwa mwezi huu kwa kubana vifaa vinavyotumika katika kilimo hicho.

Michael Books, mkurugenzi mtendaji wa Shirikisho la Wazalishaji wa mayai nchini humo, anasema sasa hakuna kuku wa kutosha nchini New Zealand ili kuendana na mahitaji.

"Kwa sasa kuna kuku milioni 3.5 wanaotaga mayai," anasema, "lakini milioni 3.9 wanahitajika ili kuhakikisha upatikanaji".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live