Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugawaji maeneo soko la Kariakoo kuwekwa wazi

KARIAKOO Ugawaji maeneo soko la Kariakoo kuwekwa wazi

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Hawa Abdulrahman Ghasia amesema bodi hiyo imejipanga kuhakikisha mradi wa ukarabati na ujenzi wa soko la Kariakoo utakamilika ndani ya muda wa mkataba na kwa ubora ambapo ugawaji wa maeneo ya biashara utakuwa wa uwazi.

Akiwa kwenye eneo la mradi huo jana Aprili 12, 2023 jijini Dar es Salaam, Ghasia ameelezea kuridhishwa kwake na kazi inayoendelea kufanywa na mkandarasi kampuni ya ESTIM construction Ltd ambapo serikali ya awamu ya sita imetoa Sh bilioni 28.03.

Akizungumzia kuhusu mchakato wa ufanyaji biashara mara baada ya mradi kukamilika, Ghasia alisema ugawaji wa maeneo ya kufanyia biashara ikiwemo maduka na vizimba utakuwa wa wazi na kwamba wananchi watapatiwa taarifa rasmi .

"Mchakato wa ugawaji maduka ,vizimba na meneo mengine ya biashara utafanyika kwa uwazi ili kila mwananchi mwenye sifa apate eneo la biashara " alisema Ghasia.

Serikali ilianza kutekeleza mradi huo wa ukarabati wa soko la zamani lililoungua na ujenzi wa soko jipya la Karikaoo Januari 2022 na utakamilika Oktoba 2023 ambapo Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) ni Mshauri Elekezi na ujenzi ukifanywa na kampuni ya ESTIM Contraction Company Ltd ambapo hadi Machi mwaka huu mradi umefikia asilimia 71.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live