Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yaipa TPDC tuzo ya heshima

Tpdc Mlk Uganda yaipa TPDC tuzo ya heshima

Sat, 2 Jul 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzani (TPDC) limetunikiwa tuzo ya heshima na Mamlaka ya Uwekezaji ya Uganda kutokana na mchango wake katika uwekezaji mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki.

Novemba 2017 aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati John Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni waliweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa bomba hilo kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Ilipofika Aprili 2021 Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu alisema, mradi huo kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani Tanzania (EACOP) utachochea uwekezaji, biashara na kufungua milango ya fursa katika nchi za Uganda na Tanzania.

Akizungumza na wanahabari leo Juni 30, 2022 Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Uwekezaji ya Uganda, Brian Tosh amesema, tuzo hiyo inatolewa kwa TPDC kwa kutambua mchango wake wa kitaalamu katika kufanikisha utekelezaji wa mradi wa EACOP.

“Mradi huu umepitia hatua kadhaa za maamuzi ambayo yalifanyika kwa kuangalia mambo mbalimbali, ikiwemo sheria na sera za uwekezaji pamoja na uzoefu wa nchi na taasisi zake.

“Uzoefu wa TPDC katika katika miradi ya ujenzi na usimamizi wa miundombinu ya mafuta na gesi, umekuwa ni mchango wenye thamani ya kipekee katika majadliano n ahata wakati wa huuambapo mradi wa EACOP uko katika hatua ya utekelezaji,” amesema Tosh.

Advertisement Alibainisha kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi, yamesababisha nchi hizo mbili kuangalia ni namna gani ya kusonga mbele.

“Bomba hili la mafuta lina mchango mkubwa hasa kwenye sekta ya uwekezaji, hivyo tunaimani na TPDC watatusaidia kuongeza mchango Uganda kupitia bomba hili,” amesema.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz