Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yaanza kutumia Bandari ya Dar kusafirisha mafuta

Bei Ya Mafuta Yapanda Huku Israel Ikitathmini Majibu Shambulio La Iran Uganda yaanza kutumia Bandari ya Dar kusafirisha mafuta

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Mafuta la Uganda (UNOC) limetangaza kuanza kutumia Bandari ya Dar es Salaam katika kupakia bidhaa hiyo kwa ajili ya kupeleka nchini kwao.

Awali UNOC ilikuwa ikitumia bandari ya Mombasa nchini Kenya katika kuchukua bidhaa hizo huku ikisafirisha kwa kutumia Shirika la Bomba la Kenya (KPC).

“Uganda imepanga kusafirisha takriban lita milioni 36 za mafuta kila mwezi (mizigo 1,028 ya lori) kupitia bandari ya Dar es salaam, “imeeleza taarifa hiyo ya UNOC iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Proscovia Nabbanja

Hata hivyo, UNOC imesema kiasi hicho kinatarajiwa kuongezeka kadri siku zinavyoenda.

“Kundi la kwanza la lita milioni 18 (malori 520 ya lori) za mafuta zilianza kupakiwa wiki hii jijini Dar es Salaam na litawasili Kampala siku zijazo,”imesema taarifa hiyo.

Makubaliano kati ya Bandari ya Dar es Salaam na Shirika la Mafuta la Uganda (UNOC) yalifanyika Mei 24 hadi 25, 2024 wakati wa Mkutano wa Pili wa Biashara kati ya Uganda na Tanzania uliofanyika Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, nchi hizo mbili zilikubaliana kuboresha njia za usafirishaji wa mafuta na bidhaa nyingine kupitia Bandari ya Dar es Salaam badala ya Mombasa, Kenya.

Uamuzi huu ulifikiwa kutokana na mabadiliko ya kiufundi na gharama katika usafirishaji wa mafuta kupitia bandari ya Mombasa, na hivyo Uganda ikaamua kuongeza matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam kama njia mbadala ya usafirishaji wa mafuta.

Katika mkutano huo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dk Doto Biteko alisema lengo la makubaliano ya mkutano huo ni kuimarisha uhusiano wa kiuchumi.

“Mkutano huu umelenga kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, hususan katika sekta ya nishati na viwanda ambayo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha miundombinu na kuongeza ushirikiano katika nyanja za biashara na viwanda,”alisema Dk Biteko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live