Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda kuzindua kiwanda cha mabasi ya umeme

Volvo Electric Bus Uganda kuzindua kiwanda cha mabasi ya umeme

Fri, 16 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujumbe wa waandishi wa habari kutoka Tanzania ukiwa umeongozana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA ) Priscus Joseph upo nchini Uganda kwa ajili ya maonesho ya magari yanayotumia umeme yanayotarajiwa kufanyika kesho Agosti 16, 2024 yakishirikisha wadau wa sekta ya magari zaidi ya 250 kutoka mataifa mbalimbali.

Ukiwa nchini Uganda ujumbe huo umepata fursa ya kutembelea kiwanda cha kwanza cha kutengeneza mabasi ya abiria ya umeme kwa Bara la Afrika cha Kiira Motors kilichopo Jinja, ambacho ujenzi wake umefikia asilimia 95, ambacho kinamilikiwa na Serikali ya nchi hiyo kwa asilimia 100.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiira Motors Paul Isaac Musasizi ameueleza ujumbe huo kutoka Tanzania kuwa kiwanda hicho kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mabasi ya abiria ya umeme takribani 5,000 kwa mwaka na hivyo kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji hasa kwa magari yanayotumia nishati ya dizeli na petroli.

Amesema kiwanda hicho ni fursa kwa nchi za Afrika hasa katika eneo la mnyororo wa uzalishaji, akiweka bayana kuwa kwa sasa asilimia 15 ya malighafi ya utengenezaji wa mabasi hayo inatoka uganda huku lengo likiwa ni kuhakikisha asilimia 60 ya malighafi ya utengenezaji wa mabasi hayo ya umeme inatoka Afrika.

Hadi kukamilika kwake kiwanda hicho kitagharimu takribani Dola Milioni 85 za Kimarekani na kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi Oktoba mwaka huu ambapo mpaka sasa ajira zaidi 700 zimeshatolewa na kiwanda hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live