Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda, Vitol Bahrain waichagua bandari ya Dar kuingizia mafuta

Bandari Kavu (600 X 303) Uganda, Vitol Bahrain waichagua bandari ya Dar kuingizia mafuta

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Uganda pamoja na kampuni ya Vitol Bahrain E.C wameichagua bandari ya Dar es Salaam kuingizia mafuta ikiwa ni miongoni mwa juhudi za kukuza uhusiano wa kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya kampuni ya Vitol E.C kupata kibali cha kusambaza mafuta nchini Uganda kilichotolewa na Kampuni mpya ya mafuta iliyoundwa na serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kusimamia uingizaji na usambazaji wa Mafuta ya Uganda National Oil Company (UNOC).

"UNOC na Vitol Bahrain E.C wamekubaliana mkataba wa miaka mitano na ushirika huu utadhamini kifedha biashara kwa kuandaa mtaji wa uwezo wa ufanyaji kazi kwa kusapotiwa na akiba yake ya kidunia na kufanya kazi na UNOC kuhakikisha ushindani wa bei ya bidhaa za mafuta.

"Kuhakikisha usalama wa usambazaji, ushirika huu unahakikisha kwamba kutakuwepo na akiba ya kutosha Uganda na Tanzania ambayo itatumika ikiwa kutakuwa na usumbufu wa usambazaji nchini. Pia mshirika ameahidi kusaidia gharama za ujenzi wa uwezo wa ziada kwa kushirikiana na UNOC wa lita 320 katika eneo la Namwambula, Mpigi," amesema Waziri madini na nishati wa Uganda, Dokta Nankabirwa Sentamu.

Vitol ni mshirika (ikiwa na mapato ya Dola 505 bilioni kwa mwaka 2022) na mfanyabishara huru wa kwanza wa kimataifa aliyeahidi kujenga uwezo wa UNOC katika biashara hii ambapo pia ataisaidia kujenga uwezo unaohitajika wa kuchukua bidhaa za petroli kutoka kiwanda cha kusafishia mafuta cha Uganda.

Serikali ya Uganda iliamua kuipa jukumu UNOC kusimamia uingizaji na usambazaji wa mafuta wa kampuni zinazojihusisha na jukumu hilo kama utekelezaji wa sheria ya usambazaji wa petrol ya mwaka 2003 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023.

Serikali ya Uganda kupitia kwa waziri nwake wa nishati, inaishukuru Tanzania chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan, kwa kupokea ujumbe maalum wa Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, Jumapili, Novemba 5 jijini Dar es Salaam na kuahidi ushirikiano mkubwa katika sekta ya nishati

Uganda imechagua bandari ya Dar es Salaam Ikiwa ni ishara ya ufanisi wa bandari na mfumo mzuri wa uingizaji nishati ya Petroli na gesi.

Hatua hii inategemea kuwa ni suluhisho la uhakika katika upatikanaji wa mafuta nchini Uganda na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Serikali ya Uganda , shehena hiyo ya mafuta italetwa kwa ushirikiano wa kampuni ya Unoc ( Uganda ) na Vitol (Bahrain )

Mkataba huo utakua ni wa miaka mitano na inatarajiwa Vitol kutumia uzoefu wake, uwezo wa kiufundi na uwekezaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live