Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufugaji wa samaki kuongeza Malighafi viwandani

Fishfarm1 Ufugaji wa samaki kuongeza Malighafi viwandani

Sun, 3 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema uwekezaji wa ufugaji wa samaki utasaidia kuongeza malighafi kwenye viwanda vya uchakataji wa samaki pamoja na kuanzisha viwanda vipya hususan katika Ukanda wa Bahari ya Hindi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Mashimba Ndaki amesema hayo wakati alipotembelea shamba la ufugaji samaki linalomilikiwa na Kampuni ya Tanlapia lililopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, ikiwa ni sehemu ya kuona shughuli zao za ufugaji wa samaki na namna wadau ambao serikali inataka wafanikiwe katika ufugaji wa samaki ili kufikia lengo la kuzalisha samaki kwa wingi ifikapo mwaka 2025 na kufikia kiwango sawa cha samaki wanaovunwa kupitia maji ya asili.

Waziri Ndaki ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuhakikisha inaendeleza wawekezaji hapa nchini ili kufikia malengo ya uzalishaji mkubwa wa samaki kupitia ufugaji wa samaki.

Aidha amesema mwelekeo wa serikali ni kuwatia moyo wazalishaji wakubwa wa samaki ili uwekezaji uwe na tija kwa taifa kwa kupatikana kwa chakula na ajira kwa nchi.

Amesema kupitia shamba la Tanlapia ambalo katika awamu ya kwanza linatarajia kuwa na mabwawa 48 ya samaki, kuwa shamba darasa la watu kutoka maeneo mbalimbali nchini kujifunza namna ya ufugaji wa samaki kibiashara.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Nazael Madala, amesema teknolojia inayotumika kwenye ufugaji samaki katika shamba la Tanlapia unaweza kufuga samaki wengi kwa kuwa ina mfumo wa kusafisha maji hayo na kuwa na uwezo wa kufuga samaki wengi kwa wakati mmoja na kufungua fursa ya kufuga samaki wengi katika eneo dogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live