Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufafanuzi wa serikali kuhusu shilingi Bilioni 50 za mahindi

Mahindi Serikali yatoa ufafanuzi bilioni 50 za mahindi

Wed, 15 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu zoezi la ununuzi wa mahindi mara baada ya Wizara ya fedha na Mipango kutoa bilioni 50 kwa ajili ya kuwa wezesha wakulima kuuuza mazao yao chini ya Wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula NFRA.

Ufafanuzi huu umetolewa na Waziri wa kilimo, Adolf Mkenda aliyefafanua kuwa fedha hizo zitaanza kwa kununua mahindi mengi katika mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Songwe, pamoja na Katavi.

"Bilioni 50 hizi wamegawa, watanunua mahindi katika mikoa ifuatayo, Ruvuma watanunua mahindi mengi, ikifuatiwa na Rukwa, Songwe, Mbeya, Katavi pamoja na Iringa, NFRA watanunua mahindi katika maeneo hayo, na kwa kila kilo moja itakuwa ni shilingi mia tano tu"-Waziri wa Kilimo.

Aidha amefafanua kuhusu vigezo vilivyowekwa katika kufanya manunuzi hayo, kuwa ni lazima wakulima wawe katika vikundi vilivyosajiliwa.

"Watanunua mahindi kupitia kwenye vikundi vilivyosajiliwa, pili kwa mkulima mmoja mmoja au mkulima mdogo hataruhusiwa kuuza zaidi ya tani 30 au gunia 300" Amesisitiza Waziri huyo.

Ametolea ufafanuzi suala la ununuzi wa mahindi unaofanywa na bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko CPB, iliyokopa shilingi bilioni 50 kutoka benki kwa ajili ya kununua mazao kwa wakulima.

"Kwanza watanunua katika mkoa wa Ruvuma tani elfu 65, alafu watanunua katika mikoa mingine kama rukwa, songwe, manyara, na bei ya kununulia itakuwa bei ya sokoni" Waziri Mkenda

Mwisho, Mawakala wote, NFRA na CPB waliwataka wakulima kutulia na wamewahakikishia kuwa watanunua mazao yao kwani tayari wana masoko nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live